Malaria huathiri mamilioni ya watu barani Afrika. Chanjo hiyo tayari inatumika kwa mafanikio katika mataifa kadhaa ya Afrika kama vile DRC, Ghana na Kenya.
« Tunapokea chanjo hii kwa mara ya kwanza ya kupambana na malaria, mojawapo ya sababu kuu za vifo vya watoto, » alifurahi Roger Samuel Kamba, Waziri wa Afya ya Umma wa DRC, dozi 693,500 chanjo ya malaria ilipokelewa ili kuwalinda watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23.
Mwaka 2023, DRC iliripoti zaidi ya visa milioni 27 vya malaria, na kusababisha vifo 24,344. Chanjo za RTS, S/AS01 na R21/Matrix-M zinapendekezwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ili kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huu hatari.
Malaria huathiri mamilioni ya watu barani Afrika. Chanjo hiyo tayari inatumika kwa mafanikio katika nchi kadhaa za Afrika kama vile Ghana na Kenya.